Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Pata huduma zifuatazo" matibabu na chanjo kwa mifugo, tunasimamia miradi ya mifugo, tunatoa Ushauri kwa wafugaji, tunadesign mabanda ya mifugo, huduma ya uhimilishaji, Elimu na Vitabu vya mwongozo bora wa ufugaji, mbegu bora za mifugo +255746031005 KARIBU SANA AFYA MIFUGO AGROVET KIBAHA PICHA YA NDEGE

CHANGAMOTO NA NJIA MBADALA KATIKA UFUGAJI


SABABU ZINAZOFANYA WAFUGAJI/WAJASIRIAMALI WENGI, KUSHINDWA 
KUFIKIA MALENGO?*

1. *MAARIFA YA KUTOSHA/ UJUZI SAHIHI.*
Watu Wengi wanakimbilia ufugaji/kilimo baada ya kuona majirani na marafiki zao wamepata mavuno bora na yenye faida. Watu wa aina hii hawatengi muda wao wa kujifunza kuhusu mienendo ya soko na mahitaji na uzalishaji wa bidhaa na mazao ya mifugo.

2. *KUKOSA UVUMILIVU*
Ufugaji unahitaji uvumilivu, watu wengi hukosa uvumilivu na kutaka mafanikio ya muda mfupi,Kutaka sana mradi ambao unakukidhi kipato cha papo hapo. Wanataka kuwa mamilionea wa muda mfupi. Wafugaji wengi Hawataki kukabiliana na tatizo la udhibiti wa magonjwa ya mifugo au changamoto ya soko. Wafugaji wa aina hii wanachotaka wao ni faida zaidi na zaidi.Ni muhimu tukafahamu kuwa mafanikio ya ufugaji hayapatikani kwa njia kama hiyo, na 
usipokuwa makini unaweza kufanya kazi na kujifurahisha tu. Hakuna kitu kizuri kinachokuja kwa urahisi. Ni lazima kufanya kazi kwa bidii na kufanya ufugaji kama ajira.


3. *GHARAMA KUBWA ZA CHAKULA CHA MIFUGO NA PEMBEJEO MUHIMU.*
Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwenye miradi ya ufugaji. Gharama za 
uendeshaji/uzalishaji wa mifugo na bidhaa za mifugo zimeongezeka sana kutokana na bei ya chakula na vifaa muhimu. Inakadiriwa kuwa Zaidi ya 70% ya gharama za uzalishaji zinatokana na chakula cha mifugo. Kutokana na hali hii ReSta AgroVET tunawashauri wakulima kutumia ubunifu na kuboresha vitu hivi ili kupunguza gharama za uzalishaji, kwa mfano kwenye vinywesheo na vilishio mfugaji unaweza kutumia ndoo, makopo au mbao badala 
ya kununua vifaa vya bei kubwa.

4. *UKOSEFU WA SOKO LA MIFUGO NA BIDHAA ZAO.*
Hii hupunguza kasi ya ufugaji lakini pia huvunja moyo wa mfugaji anayefuga kwa tija. Inavunja moyo sana kumuona mfugaji mwenzako anajitahidi kufanya mradi wa ufugaji kwa kutumia nguvu nyingi na muda mwingi na Kujikuta anaishia kukutana na soko lisilokidhi mahitaji yake na kuuza kwa bei ya hasara asiyotarajia.


5. *UKOSEFU WA USIMAMIZI NA WATAALAMU WA KUTOSHA.*
Wafugaji wengi wanapokosa mtaalam mwenye taaluma husika kwa ajili ya usimamizi wa mradi wa ufugaji, hujikuta wanaishia kufuga kwa majaribio, makosa na gharama kubwa kisha kushindwa kufikia malengo. Kwa sababu hii wanaishia kuwakatisha tamaa wenzaona hawawezi kupambana na changamoto kama vile magonjwa ya mifugo na wanapoteza kipato 
kikubwasana.
Tunaweza kuwa tunawataalamu wa mifugo wengi sana lakini hatuwatumii ipasavyo ili kuongeza tija kwenye ufugaji.


6. *MLIPUKO NA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA MIFUGO.*
Ni hasara kubwa sana inayotokana na ujuzi usio sahihi juu ya uwezo wa kudhibiti magonjwaya mifugo. Wafugaji/wakulima wengi hawana mazoea ya kufuata ratiba ya mipango ya chanjo 
na njia za usalama (bio security) na kusababisha vifo vingi vya mifugo na gharama kubwa za matitabu ndani ya muda mfupi. Wafugaji wanapaswa kutumia wataalam wa uhakika na kuepuka vishoka wanaochangia katika uharibifu wa mradi wako wa ufugaji.


7. *MWENENDO WA SOKO NA UWEZO WA KULIHUDUMIA SOKO.*
Wafugaji wengi hawana taarifa sahihi juu ya mwenendo wa soko la bidhaa za mifugo, na wamekosa ujuzi juu ya mbinu sahihi za kulihudumia soko, hivyo wengi hufuga kwa kubahatisha hali ya soko na wengine huwatumia madalali wakati wa kutafuta soko na mauzo. 
Pia soko zuri linahitaji uwezo wa kulihudumia wakati wote na kwa ubora ule ule. Wafugaji wengi huweza kuhudumia soko kwa kipindi Fulani na kuna wakati wanaishiwa na bidhaa, hii inasababisha kupoteza uaminifu wa kulihudumia soko.


8.) *KUPOTOSHWA NA WAFUGAJI WENZAKE.*
Baadhi ya wafugaji wenyewe kwa wenyewe hutengeneza uadui katika ushindani, japo ni kwelikwamba baadhi ya wafugaji wengi wana uzoefu katika ufugaji lakini wengine wanataka kupata mafanikio wao tu. Kwa kutumia nafasi hiyo wanaweza kukudanganya endapo utawauliza wanafanyaje hadi wanafanikiwa? 
Pia mfugaji mwingine anaweza kuwa na nia njema na wewe akakushauri vizuri lakini kuna tofauti sana kati mnyororo mzima utakaopitia katika ufugaji hivyo wenda aliyokushauri yasifanye kazi kwa mfugaji asiyekuwa na ujuzi. Ni vema kushauriana na mtaalamu utakuwa ili 
kuepuka hasara kubwa.
 ReSta AgroVET Tunawashauri wafugaji kuchukulia ufugaji kama 
taaluma na kuacha kutarajia mafanikio bila kutumia taaluma 

*ReSta AgroVET* *TUNAWASHAURI WAFUGAJI WA KISASA KUBADILIKA NA 
KUACHANA NA UFUGAJI WA KIZAMANI USIOKUWA NA FAIDA KUBWA*
*Wafugaji wanaweza kufanya hivi;*


1.) *Tafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wenye taatuma husika.* Wafugaji wenye uzoefu wanaweza kuwa wa msaada kwako lakini mtaalamu atakusaidia kuwa na mafanikio zaidi. 
Mitandao ya kijamii inaweza kusaidia wafugaji kununua au kuuza bidhaa zao na kushirikikatika kutoa mawazo na changamoto lakini ni lazima ielewe kuwa kuwa, mfugaji makini hafanyi ugunduzi na matibabu ya magonjwa kwa online (Achana na Vishoka pata, huduma ya uhakika). Ni vizuri Mtaalam wa mifugo atembelea shamba lako na kutoa huduma.


2.) *Daima tafuata taarifa sahihi za soko na masoko ya bidhaa/mifugo yako kabla ya
uzalishaji na kabla ya kufikia muda wa kuuza bidhaa zako*. e.g nyama na mayai. Maarifa ni 
muhimu.


*3.) Wafugaji wajitahidi Kupunguza gharama za uzalishaji kwa kadri iwezekanavyo kwa kutumia bidhaa nafuu lakini zenye ubora wa juu*


4.) *Jitahidi kwenda semina na mafunzo ya ufugaji kwa kila wakati unapopata fursa.* Hii itakusadia kufahamu mambo mengi Zaidi na teknolojia na mbinu mpya zinazotumika kwenye ufugaji. Kupata maarifa hakukuletei hasara bali hukupa faida. Wafugaji wengi hupotezwa na wafugaji wenzao na vishoka wanaopatikana kila kona. Jitahidi kupata maarifa kwa sana na
kuwa karibu na mtaalamu wa mifugo wa uhakika na aneaminika

5.) *Pata mifugo kuanzia mradi kutoka kwenye Chanzo kinachoaminika na kuthibitika.* Kwa kutumia msaada wa mtaalam mfugaji unaweza kufahamu aina nzuri ya mifugo unayohitaji, na kujua historia ya vizazi vilivyopita kizazi hadi kizazi, ubora wa uzalishaji na kiwango chake. Epuka inbreeding yani kuzalisha kizazi cha ukoo mmoja mara nyingi Zaidi ya 
kizazi cha tatu hupunguza ubora na kusababisha, udumavu na mwishoni uzalishaji uliopungua.

*SOMA FUGA TIMIZA MALENGO*



IMEANDIKWA NA Dr RIZIKI NGOGO (VET)
 ReSta AgroVET 
 0763222500/ 0652515242
 restaagrovet@gmail.com

www.afyamifugo.wixsite.com/agrovet

http://www.afyamifugo.blogspot.com/

http://www.instagram.com/resta_agrovet/

http://www.facebook.com/AfyaMIFUGOtz/

 Morogoro, Tanzania.

Katika kukabiliana na changamoto hizo hapo juu..

KARIBU!  ReSta AgroVET
Sasa tunatoa huduma ya Kusimamia miradi ya ufugaji/Mifugo/farms kwa *(ROUTINE/WEEKLY/MONTHLY FARM VISIT FOR GENERAL ANIMAL HEALTH CARE)* Pamoja na Udhibiti wa Magonjwa kwa gharama ndogo. Ili kuwasaidia wafugaji kutimiza malengo yao hatua kwa hatua.

Popote ulipo utazipata Huduma zetu zote za mifugo kutoka kwa wataalam wetu waliosajiliwa popote ulipo tunakufikia.


 http://www.instagram.com/resta_agrovet/

http://www.facebook.com/AfyaMIFUGOtz/

http://www.afyamifugo.blogspot.com/

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MCHANGANUO WA FEDHA, UFUGAJI WA KUKU

*JE NI KIASI GANI CHA FEDHA INAYOHITAJIKA KUANZISHA UFUGAJI WA KUKU?*

HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)

UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA  SIKU YA 1 -5:            WAPE GLUCOSE NA MCHANGANYIKO MMOJAWAPO KATI YA HII IFUATAYO:-

FAHAMU UMUHIMU WA MADINI YA CALCIUM NA PHOSPHORUS KWA MIFUGO

*FAHAMU UMUHIMU WA DCP KWA MIFUGO.* DCP=Dicalcium Phosphate ✅*DCP ni nini ?* DCP ni mchanganyiko wa madini ya Calcium na Phosphorus. DCP husaidia wanyama wenye upungufu au maradhi yatokanayo na ukosefu wa madini haya ya Calcium na Phosphorus ✅FAIDA KWA KUKU: Huzuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini, huimarisha maganda ya mayai, Pia husaidia utagaji wa mayai ✅FAIDA KWA WANYAMA WENGINE: Huzuia ng’ombe kuanguka, viungo dhaifu na huimarisha mifupa na kupunguza matatizo ya mifupa. 📞Dr Riziki Ngogo(DVM) ☎*AfyaMIFUGO Tz*        0763222500     afyamifugo@gmail.com     afyamifugo.blogspot.com

UFUGAJI WA SUNGURA

SIFA ZA BANDA ZURI LA SUNGURA                                  i.             Liweze kuingiza hewa ya kutosha                                ii.             Liwe na miundombinu inayorahisisha wakati wa kusafisha                               iii.             Lisiwe na ncha kali (weka wavu kwenye sakafu)           ...

KWA WAFUGAJI WA MBWA, WAUZAJI NA WANUNUZI

FAHAMU HATUA ZA UKUAJI WA MBWA NA HUDUMA MUHIMU HATUA KWA HATUA ✅ 1-4 Wiki *⃣Macho na masikio hufungua siku ya 10.  *⃣Siku ya  15 mbwa anaweza kusimama. *⃣Siku ya 20 mbwa anaanza kujifunza kutembea. Watoto bado wanahitaji sana kuwa karibu na  mama. *⃣Kwa Kawaida  hata kama puppy mbwa mtoto ana afya. Chukua mtalamu wa mifugo  siku ya 1 au 2 ili aangalie matatizo ya kuzaliwa. *⃣Mikia inaweza kukatwa katika umri huu. kucha zinaweza kukatwa pia *⃣Puppy mbwa mtoto anajifunza kuwa na uhusiano na mama na mahusiano ya karibu na wengine baadaye.

UFUGAJI WA NGURUWE

*UFUGAJI WA NGURUWE (PIG FARMING)* 🐖🐖🐖🐖🐖🐖🐖🐖 Watu wengi wameanzisha miradi ya ufugaji lakini wamejikuta wameingia kwenye vikwazo vingi vinavyo warudisha nyuma na kushindwa kufikia malengo na kilele cha mafanikio kwa muda uliopangwa. *Suluhisho kubwa ni kupata ujuzi wa muhimu unaotakiwa/hitajika kwa muda mwafaka kabla na wakati wote wa uendeshaji wa miradi ya ufugaji* UJUZI HUO NI PAMOJA NA VITU MUHIMU VILIVYOTAJWA HAPA

SABABU ZA KUKU KUNYONYOKA MANYOYA

_UFANISI WA KUKU_ Fahamu kuwa, kwa kawaida kuku hunyonyoka manyoya na kuota manyoya mapya  katika vipindi tofauti vya ukuaji wa kuku. *_Moulting_* Kunyonyoka manyoya na kubadilisha manyoya mapya hutokea kuku akiwa na umri wa kianzia wiki ya 4-5, wiki ya 8, Wiki ya 13, Wiki ya 20. Pia angalau mara moja kwa kila mwaka akifikia umri wa utagaji. Visababishi vingine vinavyochangia kunyonyoka manyoya na kuota manyoua mapya ni pamoja na _mabadiliko na upungufu wa chakula, mabadiliko ya kimsimu ya hali ya hewa, mabadiliko ya ghafla ya mwanga_ n.k Tambua kuwa kunyonyoka manyoya kunaweza kuathiri ufanisi wa kuku katika ukuaji/kuongezeka uzito na utagaji, hivyo unashauriwa kufanya yafuatayo, _1. Punguza stress kwa kuku._ _2. Tumia chakula bora chenye protein ya kutosha._ _3. Epuka mabadiliko ya ghafla kwenye mwanga, chakula n.k._ ●By Dr Riziki Ngogo      0763222500    #ReSta AgroVET    #FARMERS Platform    # INTERCHICK- ...

UFUGAJI WA MBWA (PETS)

Kwa nini tunafuga Mbwa? 1⃣. Malengo ya Usalama Nyumbani, Polisi 2⃣kuondoa upweke na kutoa kampani: -Pets 3⃣Uwindaji 4⃣Mashindano na burudani ya maonyesho ya Mbwa (Greyhounds) 5⃣Uongozi wa vipofu. (Mbwa mwongozo) Kwa ujumla Mbwa nchini Tanzania wengi ni jamii ya Mbwa Asili wa kiafrika kama MONGREL

GERMAN SHEPHERD Mbwa wa kizungu fahamu asili yake na matumizi yake

Fahamu asili ya Mbwa wa kizungu GERMAN SHEPHERD. Asili yake ni nchini Uingereza na Ireland. Huko walitumika katika kazi za Uchungaji wa Mifugo huko Ujerumani miaka ya 1899. Moja ya kazi kubwa walitumika kama mbwa wanaofanya kazi zilizotengenezwa awali kwa ajili ya kuchunga kondoo. Tangu wakati huo kutokana na nguvu zao, akili, ujuzi, na utii, wachungaji wa Ujerumani ulimwenguni kote mara nyingi hupendelea aina hizi za Mbwa, ikiwa na pamoja na kupata msaada wa ulemavu, kutafuta wezi-na-kuwaokoa watu, kazi za kipolisi na majukumu ya kijeshi, na hata katika maonyesho mbalimbali. By Dr Riziki Ngogo        0763222500       afyamifugo@gmail.com UFUGAJI NI MAARIFA

*DHIBITI UGONJWA WA KIDELI/MDONDO (Newcastle) KWA KUKU* AfyaMIFUGO🇹🇿:

  UFUGAJI NI MAARIFA *DHIBITI UGONJWA WA MDONDO/KIDELI (Newcastle) KWA KUKU* [Part 1 AfyaMIFUGO🇹🇿:)*DHIBITI UGONJWA WA KIDELI (Newcastle) KWA KUKU* [Part 1 AfyaMIFUGO🇹🇿:) *Kideli/MDONDO (Newcastle) ni nini* ❓  🐓Huu ni ugonjwa hatari kwa ufugaji wa kuku unaosababishwa na virusi. 🐓ugonjwa huu huathiri sana kuku mfumo wa kupumua, na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mayai na vifo vingi kufikia 100% kwa kuku wagonjwa.
TUNATOA USHAURI HATUA KWA HATUA KUHUSU UFUGAJI, HUDUMA ZA MATIBABU KWA MIFUGO, TUNABUNI RAMANI ZA MABANDA YA MIFUGO KULINGANA NA AINA YA MIFUGO, MAFUNZO YA MBWA, UFUGAJI KWA MTU BINAFSI NA VIKUNDI HUDUMA ZA CHANJO KWA MIFUGO,KANUNI/FORMULA NZURI ZA VYAKULA VYA MIFUGO TUNASIMAMIA MASHAMBA YA MIFUGO (FARM), TUNATOA MCHANGANUO WA FEDHA UNAOHUSIANA MIRADI YA UFUGAJI 0763222500

PATA MAARIFA FUGA TAJIRIKA

JIWE LA MADINI/ MINERAL BLOCK

FARMERS PLATFORM PATA MAARIFA, FUGA, TIMIZA MALENGO Bonyeza hapa kutazama bidhaa Kwa nini Jiwe la Madini ni muhimu kwa Wanyama? Kwa kukosekana kwa chumvi chumvi na madini; hamu ya kula hupungua, ukuaji hupungua, uzalishaji wa maziwa na nyama hupungua, matatizo ya uzazi yanaweza kupatikana, mfumo wa kinga (mfumo wa ulinzi) hudhoofika na wanyama hushambuliwa na magonjwa. Kukosa madini haya kunaweza kupeleka tabia zifuatazo kwa wanyama; kula na kulamba vitu visivyo vya chakula (jiwe, udongo, mfupa, sachet, nguo, nk)  Wanyama hutumia  JIWE LA MADINI/ MINERAL BLOCK Mfululizo kwa ajili ya kufidia kiasi Cha madini kilichopungua mwilini. Kesi za kuhara zinazotokana na tabia hizi pia huzuiwa ikiwa mnyama atapata madini inavyopaswa. Kiasi cha Matumizi: matumizi ya kila siku kwa MINERAL BLOCK;  Ng'ombe kila siku 80 gr / siku,  Kondoo, mbuzi 5-15 gr / siku. Bonyeza hapa kutazama bidhaa Why Mineral Block in Animals? In the absence of salt and mineral matter; appetite decreases, g...

FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU.

FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU. Dume la Sungura linauwezo wa kutumika vizuri kwa kupandisha majike ya sungura baada ya miezi 8. Kabla ya kutimiza mwaka 1 Anaweza kupanda sungura  jike 1 kila baada ya siku 3 au 4. Na baada ya kufikia umri wa miezi 12 (mwaka1) na zaidi anauwezo wa kutumika kupandisha majike 4-6 ndani ya siku 7 (wiki1). Sungura madume waliozeeka wwnye umri kuanzia miaka 6 na zaidi hawatakiwi kutumika kwenye uzalishaji kwani ubora wa nguvu zao hupungua kufikia umri huo. Kitalaam unashauriwa kuhakikisha sungura wako wa mbegu anapata nyongeza ya chakula chenye virutubisho aina ya  protein, Vitamini na Madini  ili kuwafanya wawe na afya nzuri wakati wote. Pia unashauriwa kutowwka madume ya mbegu zaidi ya mmoja ndani chumba au banda moja kwa sababu madume wanatabia ya kupigana na kuumizana vibaya pindi wanapokaa pamoja. by Dr Riziki Ngogo FARMERS Platform 0763222500 0652515242 Follow zaidi http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http:...

INCOME COMES FROM PRODUCTS OR SERVICES, EVERYONE IS DOING A BUSINESS

ARE YOU EMPLOYED? INCOME COMES FROM PRODUCTS OR SERVICES The type of product or services you are selling determines the income you will make. If you work for an employer, you are in business already. You wake up each day and have 8 hours of 1 day of work to sell your service, you've got one client who bulk buys all of them  (your product/services) for the year and uses them to fulfil their ambition. This, is a limiting way to earn money, because you can only sell your service/product time once, to one buyer. A better way would be to figure out why they are buying your time, what problems you are solving for them, and then develop products and services that many people can buy. START YOUR OWN FARM, WE ARE HERE TO ASSIST YOU STEP BY STEP instagram Facebook Our blog 0652515242 0754031039 CC FARMERS Platform ReSta AgroVET ReSta Dietetics and Counseling CHOICELINE Ltd FARMERS PLATFORM PATA MAARIFA, FUGA, TIMIZA MALENGO

NG'OMBE BORA WA MAZIWA FOR SALE

JIPATIE MITAMBA BORA  YA NG'OMBE WA MAZIWA Umri = miaka 2 Heifer Hali yake mwa sasa=  Hana mimba Aina = Friesian Uzalishaji wa maziwa= Mama ana Record nzuri Mawasiliano Simu 0763222500 Email afyamifugo@gmail.com UNGANA NASI ZAIDI KUPITIA http://www.instagram.com/farmers_platform/ http://www.facebook.com/farmersplatform/ http://www.afyamifugo.blogspot.com/ https://farmersplatform.site123.me/

MBOLEA/ FOLIAR FERTILIZERS

BONYEZA HAPA KUONA BIDHAA ZINGINE Kwanini mbolea ya Booster? Booster ni mbolea kamili ya mimea iliyo na virutubishi vyote muhimu kwa ukuaji wa mmea wenye afya na mavuno bora. Imetengenzwa  maalumu ili kuweza kufyonzwa haraka kupitia majani ya mmea. BONYEZA HAPA KUONA BIDHAA ZINGINE Why Booster Fertilizer? Booster is a complete foliar fertilizer containing all the major macro and microelements essential to healthy plant growth and optimum yields. Booster formulated for rapid absorption through the leaves. BONYEZA HAPA KUONA BIDHAA ZINGINE

Farmers Platform


Minyoo kwenye mbuzi (cyst from goat)

PLASTIC BAGS

PLASTIC BAGS
Mifuko ya plastiki ni hatari kwa mifugo yako. Huleta hasara na kushuka kwa uzalishaji wa kipato (Pile of bags more than 1Kg removed from one goat kama tunaweza kuona afya isiyoridhisha kwa huyu mbuzi

FRACTURE IN CATTLE

FRACTURE IN CATTLE
Management of fracture

UFUGAJI WA KUKU KWA TIJA

UFUGAJI WA KUKU KWA TIJA
KITABU CHA MWONGOZOUFUGAJI WA KUKU

UFUGAJI WA NGURUWE KWA TIJA

UFUGAJI WA NGURUWE KWA TIJA
KITABU CHA MWONGOZO BORA UFUGAJI WA NGURUWE, TENGENEZA FAIDA NDANI YA MUDA MFUPI

FUGA KWA TIJA

FUGA KWA TIJA
Fahamu kanuni za lishe bora kwa mifugo yako

MBINU ZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

MBINU ZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
MBINU ZA UFUGAJI

Mimea hii ni sumu kwa mifugo yetu husababisha vifo vya ghafla

Mastitis in goat