i.
Liweze kuingiza hewa ya kutosha
ii.
Liwe na miundombinu inayorahisisha wakati wa
kusafisha
iii.
Lisiwe na ncha kali (weka wavu kwenye sakafu)
iv.
Weka mataulo chini kwa ajili ya kulalia na
wakati wa kujifungua
v.
Weka maboksi ya kujificha sungura
vi.
Zungushia wavu ili kuzuia wanyaa wengine kama
mbwa, paka na panya wanaweza kuwala sungura
vii.
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula na maji
UTOAJI WA CHAKULA NA MAJI
Tumia majani na mboga mboga pia mabaki ya jikoni ya mboga,
Tumia chakula cha
kuku kama pumba au chakula kilichochanganywa kinachotumika kukuzia kuku
wanaokua ili kuhakikisha sungura wako wanapata virutubisho vya kutosha
Kwa upande wa MAJI hakikisha unawapa maji masafi na salama kila siku na kuhakikisha usafi wa vyombo vya
kuwekea maji na chakula.
Zingatia
usafi wa mabanda kwa ujimla, badilisha matandazio (mataulo)
yaliyochoka mara moja kila wiki, umakini unahitajika wakati wa kufanya usafi
MANYOYA YA SUNGURA WAZAZI huongezeka sungura wapokaribia kujifungua hayatakiwi
kuondolewa.
Usitumie sungura wazazi wa aina moja (kaka na dada) kwenye
kuzaliana kwa muda mrefu
HUDUMA ZA MUHIMU KWA SUNGURA
·
Kuhasi sungura madume ambao hawatumiki kama
wazazi ili kuepuka tabia za kugombana
·
Kukata kucha na meno ili kupunguza urefu
·
Dawa za kuua wadudu kama viroboto
·
Dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
KWA MSAADA ZAIDI HATUA KWA HATUA WASILIANA NA……….
AfyaMIFUGO Tz
Riziki Ngogo (Vet Doctor)
0763222500/ 0652515242
afyamifugo@gmail.com
afyamifugo.blogspot.com
Ninao sungura wawili tu ambao ni kaka na dada je wanaweza kuzaliana!!?
JibuFuta1. Kama ndio naomba ushauri nini cha kufanya ili wazaliane maana ninao kwa muda sasa na sioni dalili za kuzaliana
2. Ni wakati gani sahihi wa sungura kupandiana na natakiwa kufanyaje ili wapandiane na nitajuaje kuwa mimba imeingia