Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Pata huduma zifuatazo" matibabu na chanjo kwa mifugo, tunasimamia miradi ya mifugo, tunatoa Ushauri kwa wafugaji, tunadesign mabanda ya mifugo, huduma ya uhimilishaji, Elimu na Vitabu vya mwongozo bora wa ufugaji, mbegu bora za mifugo +255746031005 KARIBU SANA AFYA MIFUGO AGROVET KIBAHA PICHA YA NDEGE

(AI) UHAMILISHAJI/ Artificial Insemination

*KWA WAFUGAJI SOMA HII, PATA MAARIFA KUHUSU VITU VINAVYOWEZA KUKUONGEZEA FAIDA KWENYE KAZI YA UFUGAJI.*
*(AI) UHAMILISHAJI/ Artificial Insemination* inajulikana kwa wafugaji wengi kama AI, ni moja ya mbinu za kuzaliana ambazo zimechangia katika maendeleo ya sekta mifugo hasa katuka sekta ya maziwa katika nchi zilizofanikiwa kwenye ufygaji wenye tija na faida kubwa.

Mbinu ya AI  huanza na kuchagua ng'ombe wenye afya nzuri, ambao hawana ugonjwa wala kilema cha aina yoyote na wenye uwezo wa kuzalisha mazoa yake kwa kiasi kikubwa cha ubora wa juu.
Wafugaji/ Wakulima wanashauriwa kutumia mbegu zilizothibitika kutoka kwa mifugo wazazi walio thibitika ambao wanapatikana kutoka vituo vya AI na watoa huduma waliosajiliwa.



✅ *Faida za Uhamilishaji/AI*
1.Kuzuia magonjwa yanayoweza kuenezwa kutoka kwa dume.

2.Kiasi cha mbegu nyingi kinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu na kwa gharama ndogo ili kuwezesha upimaji mkubwa na uteuzi wa ng'ombe bora.

3.Inaimarisha na kuboresha maendeleo na ubora wa  maumbile kwa sababu ng'ombe bora zaidi huchaguliwa na hutumiwa kukusanya mbegu.

4. Wafugaji/wakulima wadogo wadogo kwa njia ya AI wanaweza kupata ng'ombe wazuri kwa bei nafuu 5. Mfugaji Unaweza kuchagua ng'ombe mwenye sifa unazozitaka.

6. Ni rahisi kudhibiti tatizo la inbreeding(wanyama wa koo moja kuzaliana kaka na dada) kwa mifugo.

7. Inasaidia kuongeza thamani na kipato kwa mfugaji ataboresha mifugo yake na  mazao yatokanayo na mifugo na kuuza kwa bei nzuri.



✅  *Hasara za AI/Uhamilishaji*

1.Inahitaji maarifa ya kutambua mnyama ambaye yuko kwenye joto na muda  unaofaa wa kupandikiza mbegu  ili kupata uhakika mkubwa zaidi wa kushika mimba na kuzaliwa.

2. Wahamishaji lazima wawe na mafunzo juu ya mbinu hii.

3. Inahitaji uwekezaji mkubwa katika vifaa.



*Sababu zinazoathiri kiwango cha mimba na kuzaliana kwa mbinu ya AI:*


Mnyororo wa uzazi/kuzaliana hutegebmea kutungwa kwa mimba na kuzaa kiumbe mwenye afya.
Ili Mimba  itungwe inategemea mambo kadhaa, ambayo huunda mnyororo wa kuzaliana/uzazi.
Dhana ya mnyororo ni kwamba tunazungumzia uwezo wa viungo vya mwili wa mnyama.  kama kiungo  kimoja kikiwa na shida Kwa hiyo kwenye mnyororo wa kuzaliana kutaathirika na kuathiri kutungwa kwa mimba na uwezo wa kuzaa.

✅ *Sababu zinazoathiri uzalishaji kwa ng'ombe wa maziwa*

Imekuwa ni kawaida kwa wafugaji wengi wa ng'ombe wa maziwa kutofautiana katika kiwango cha uzalishaji kutoka shamba hadi shamba na wanyama kwa wanyama.
Tofauti hii ya uzalishaji inaweza kuboreshwa kwa kutumia mbinu za kitaalam kama AI ili kuboresha ng'ombe na mazao yatokanayo na mifugo

Sababu zinazohusiana na kutofikia malengo ya uzalishaji wa maziwa.
1⃣. *Sababu zitokanazo na wanyama wenyewe:*

☑ *Jamii na koo za mnyama*
- Uwezo wa uzalishaji wa maziwa hupungua kama ifuatavyo - Friesian, Ayrshire,
Guernsey, Jersey, Sahiwal, Boran na Zebu. Hii inatokana na maumbile
Ya Genetic ya koo za mnyama.



☑ *Uhusiano wa umri wa ng'ombe*

- Ng'ombe  wakubwa zaidi ya  (>miaka  6 ) wanazalisha maziwa 25% zaidi kuliko ng'ombe wadogo kiumri.
Uzao wa Kwanza first lactation huzalisha maziwa 25% chini zaidi ya fourth lactation uzao wa nne. Pia Baada ya mavuno ya kuzalisha maziwa mengi  peak lactation kuna kushuka kwa kiasi cha uzalishaji, kutikana na ng'ombe kuingezeka umri na kuzeeka.

Hivyo mfugaji unashauriwa kipindi ambacho  uzalishaji wa maziwa unaongezeka kwa umri, shamba la ng'ombe hupaswa kuwa na wanyama wadogo ili kuboresha uzalishaji na kuwabadilisha ng'ombe waliozeeka.


 ☑ *Stage/Hatua ya uzalishaji Hatua ya uzalishaji wa maziwa stage of lactation*-
Uzalishaji wa maziwa huongezeka wakati wa miezi miwili ya kwanza kufuatia kuzaliwa kwa ndama/calving (uzalishaji kufikia kilele), kisha hupungua hatua kwa hatua baadaye.


☑ *Oestrus/siku za joto* uzalishaji wa maziwa hupungua siku ambayo ng'ombe yupo  joto au siku baada ya joto.


☑ *Mimba/Pregnancy stage-*
 Kwa ng'ombe mwenye mumva ya miezi 4
hadi mwezi wa 5 wa ujauzito, uzalishaji wa maziwa  wa ng'ombe hupungua kwa kasi zaidi.


☑ *Ukubwa wa ng'ombe*-
Ng'ombe wenye maumbile makubwa huzalisha maziwa zaidi kuliko ng'ombe wadogo wa uzao sawa na koo moja.

✅ *Sababu zinazotikana na mazingira:*

☑ *Malisho*-
Lishe ni muhimu sana na upungufu wa virutubisho, hasa protini au nishati hupunguza uzalishaji wa mazao ya maziwa.
Urefu wa kipindi ambacho ng'ombe hupunzishwa kukamuliwa.(dry period)
Kupumzisha kwa Kipindi cha muda mfupi chini ya siku (<60days) husababisha uzalishaji wa maziwa kushuka.
Hali ya ng'ombe wakati wa kuzaa - Ng'ombe waliokonda sana au  walionenepa na mafuta mengi huzalisha maziwa kidogo.


☑ *Ratiba ya ujamuaji maziwa*-
Ng'ombe wanaokamuliwa mara 3 wanazalisha maziwa zaidi ya asilimia 10-25% kuliko wale wanaokamuliwa mara mbili kwa siku.  Pia Ng'ombe wanaokamuliwa mara 4kwa siku huzalisha zaidi ya 5-15% za maziwa  walewanaokamuliwa maziwa mara tatu.

☑ *Mpangilio wa Shamba*
- Uhusiano wa mpangilio wa malisho, sehemu ya kukamulia,  seheme ya banda na sehemu ya maji.
Wanyama wanaotembea umbali mrefu watatumia nguvu/energy nyingi, ambayo wanapaswa kutumia kwa ajili ya kutengeneza maziwa.



☑ *Magonjwa*
- Magonjwa kama ya kiwele Mastitis, ketosis, milk fever na mengine huathiri uzalishaji wa maziwa.
Mabadiliko ya mkamuaji na utaratibu wa ratiba ya ukamuaji maziwa husababisha kupungua maziwa.


☑ *Hali ya hewa/Climate*
- joto kali la juu hupunguza mavuno ya uzalishaji maziwa zaidi kuliko joto la chini. joto huathiri raha ya wanyama na ulaji wa chakula.
Mifugo iliotoka kwenye mazingira ya baridi huathiriwa zaidi na joto kuliko mifugo iliyozoea mazingira ya joto. Hivyo mfugaji unashauriwa kufahamu vizuri jamii na aina ya ng'ombe unaotaka kuwafuga waendabe na mazingira halisi ili kuleta tija.
.
 #Written by Dr Riziki Ngogo(DVM) 
_____________________________________________

Jifunze mengi Fuga na  ReSta AgroVET tupo Morogoro/ Msamvu kidabaga/Mtaa wa genda/ karibu na ATM za CRDB.  Kwa daladala shuka kituo cha polisi msamvu barabara mpya ya kichangani yenye mataa iliyopo oposite na the islamic foundation Radio Imamu
0763222500
0652515242
_________________________________

The Recommended Standards for all your Animal Care needs, Veterinary Services and Products.  Pata vitabu vya mwongozo bora ufugaji wenye tija hatua kwa hatua.

__________________________________
#Fuga kwa Muda mfupi Uza Fuga tena.
#Tumia gharama kidogo pata faida kubwa.
#Jipatie kitabu kinachokupa maarifa sahihi.
#Fuga kwa tija hatua kwa hatua
SOMA FUGA TAJIRIKA.....
__________________________

KARIBU!  ReSta AgroVET
Sasa Unaweza kupata huduma zetu zote za mifugo kutoka kwa wataalam wetu waliosajiliwa popote ulipo tunakufikia.
Piga simu # 0763222500
   Email :afyamifugo@gmail.com

http://www.instagram.com/resta_agrovet/

http://www.facebook.com/AfyaMIFUGOtz/

http://www.afyamifugo.blogspot.com/
UFUGAJI NI MAARIFA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MCHANGANUO WA FEDHA, UFUGAJI WA KUKU

*JE NI KIASI GANI CHA FEDHA INAYOHITAJIKA KUANZISHA UFUGAJI WA KUKU?*

HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)

UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA  SIKU YA 1 -5:            WAPE GLUCOSE NA MCHANGANYIKO MMOJAWAPO KATI YA HII IFUATAYO:-

FAHAMU UMUHIMU WA MADINI YA CALCIUM NA PHOSPHORUS KWA MIFUGO

*FAHAMU UMUHIMU WA DCP KWA MIFUGO.* DCP=Dicalcium Phosphate ✅*DCP ni nini ?* DCP ni mchanganyiko wa madini ya Calcium na Phosphorus. DCP husaidia wanyama wenye upungufu au maradhi yatokanayo na ukosefu wa madini haya ya Calcium na Phosphorus ✅FAIDA KWA KUKU: Huzuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini, huimarisha maganda ya mayai, Pia husaidia utagaji wa mayai ✅FAIDA KWA WANYAMA WENGINE: Huzuia ng’ombe kuanguka, viungo dhaifu na huimarisha mifupa na kupunguza matatizo ya mifupa. 📞Dr Riziki Ngogo(DVM) ☎*AfyaMIFUGO Tz*        0763222500     afyamifugo@gmail.com     afyamifugo.blogspot.com

UFUGAJI WA SUNGURA

SIFA ZA BANDA ZURI LA SUNGURA                                  i.             Liweze kuingiza hewa ya kutosha                                ii.             Liwe na miundombinu inayorahisisha wakati wa kusafisha                               iii.             Lisiwe na ncha kali (weka wavu kwenye sakafu)                              iv.             Weka mataulo chini kwa ajili ya kulalia na wakati wa kujifungua                                v.             Weka maboksi ya kujificha sungura                              vi.             Zungushia wavu ili kuzuia wanyaa wengine kama mbwa, paka na panya wanaweza kuwala sungura                             vii.             Liwe na sehemu ya kuwekea chakula na maji

KWA WAFUGAJI WA MBWA, WAUZAJI NA WANUNUZI

FAHAMU HATUA ZA UKUAJI WA MBWA NA HUDUMA MUHIMU HATUA KWA HATUA ✅ 1-4 Wiki *⃣Macho na masikio hufungua siku ya 10.  *⃣Siku ya  15 mbwa anaweza kusimama. *⃣Siku ya 20 mbwa anaanza kujifunza kutembea. Watoto bado wanahitaji sana kuwa karibu na  mama. *⃣Kwa Kawaida  hata kama puppy mbwa mtoto ana afya. Chukua mtalamu wa mifugo  siku ya 1 au 2 ili aangalie matatizo ya kuzaliwa. *⃣Mikia inaweza kukatwa katika umri huu. kucha zinaweza kukatwa pia *⃣Puppy mbwa mtoto anajifunza kuwa na uhusiano na mama na mahusiano ya karibu na wengine baadaye.

UFUGAJI WA NGURUWE

*UFUGAJI WA NGURUWE (PIG FARMING)* 🐖🐖🐖🐖🐖🐖🐖🐖 Watu wengi wameanzisha miradi ya ufugaji lakini wamejikuta wameingia kwenye vikwazo vingi vinavyo warudisha nyuma na kushindwa kufikia malengo na kilele cha mafanikio kwa muda uliopangwa. *Suluhisho kubwa ni kupata ujuzi wa muhimu unaotakiwa/hitajika kwa muda mwafaka kabla na wakati wote wa uendeshaji wa miradi ya ufugaji* UJUZI HUO NI PAMOJA NA VITU MUHIMU VILIVYOTAJWA HAPA

SABABU ZA KUKU KUNYONYOKA MANYOYA

_UFANISI WA KUKU_ Fahamu kuwa, kwa kawaida kuku hunyonyoka manyoya na kuota manyoya mapya  katika vipindi tofauti vya ukuaji wa kuku. *_Moulting_* Kunyonyoka manyoya na kubadilisha manyoya mapya hutokea kuku akiwa na umri wa kianzia wiki ya 4-5, wiki ya 8, Wiki ya 13, Wiki ya 20. Pia angalau mara moja kwa kila mwaka akifikia umri wa utagaji. Visababishi vingine vinavyochangia kunyonyoka manyoya na kuota manyoua mapya ni pamoja na _mabadiliko na upungufu wa chakula, mabadiliko ya kimsimu ya hali ya hewa, mabadiliko ya ghafla ya mwanga_ n.k Tambua kuwa kunyonyoka manyoya kunaweza kuathiri ufanisi wa kuku katika ukuaji/kuongezeka uzito na utagaji, hivyo unashauriwa kufanya yafuatayo, _1. Punguza stress kwa kuku._ _2. Tumia chakula bora chenye protein ya kutosha._ _3. Epuka mabadiliko ya ghafla kwenye mwanga, chakula n.k._ ●By Dr Riziki Ngogo      0763222500    #ReSta AgroVET    #FARMERS Platform    # INTERCHICK-  Chicken School of Excellence FARMERS PLATFORM PATA

UFUGAJI WA MBWA (PETS)

Kwa nini tunafuga Mbwa? 1⃣. Malengo ya Usalama Nyumbani, Polisi 2⃣kuondoa upweke na kutoa kampani: -Pets 3⃣Uwindaji 4⃣Mashindano na burudani ya maonyesho ya Mbwa (Greyhounds) 5⃣Uongozi wa vipofu. (Mbwa mwongozo) Kwa ujumla Mbwa nchini Tanzania wengi ni jamii ya Mbwa Asili wa kiafrika kama MONGREL

GERMAN SHEPHERD Mbwa wa kizungu fahamu asili yake na matumizi yake

Fahamu asili ya Mbwa wa kizungu GERMAN SHEPHERD. Asili yake ni nchini Uingereza na Ireland. Huko walitumika katika kazi za Uchungaji wa Mifugo huko Ujerumani miaka ya 1899. Moja ya kazi kubwa walitumika kama mbwa wanaofanya kazi zilizotengenezwa awali kwa ajili ya kuchunga kondoo. Tangu wakati huo kutokana na nguvu zao, akili, ujuzi, na utii, wachungaji wa Ujerumani ulimwenguni kote mara nyingi hupendelea aina hizi za Mbwa, ikiwa na pamoja na kupata msaada wa ulemavu, kutafuta wezi-na-kuwaokoa watu, kazi za kipolisi na majukumu ya kijeshi, na hata katika maonyesho mbalimbali. By Dr Riziki Ngogo        0763222500       afyamifugo@gmail.com UFUGAJI NI MAARIFA

*DHIBITI UGONJWA WA KIDELI/MDONDO (Newcastle) KWA KUKU* AfyaMIFUGO🇹🇿:

  UFUGAJI NI MAARIFA *DHIBITI UGONJWA WA MDONDO/KIDELI (Newcastle) KWA KUKU* [Part 1 AfyaMIFUGO🇹🇿:)*DHIBITI UGONJWA WA KIDELI (Newcastle) KWA KUKU* [Part 1 AfyaMIFUGO🇹🇿:) *Kideli/MDONDO (Newcastle) ni nini* ❓  🐓Huu ni ugonjwa hatari kwa ufugaji wa kuku unaosababishwa na virusi. 🐓ugonjwa huu huathiri sana kuku mfumo wa kupumua, na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa mayai na vifo vingi kufikia 100% kwa kuku wagonjwa.
TUNATOA USHAURI HATUA KWA HATUA KUHUSU UFUGAJI, HUDUMA ZA MATIBABU KWA MIFUGO, TUNABUNI RAMANI ZA MABANDA YA MIFUGO KULINGANA NA AINA YA MIFUGO, MAFUNZO YA MBWA, UFUGAJI KWA MTU BINAFSI NA VIKUNDI HUDUMA ZA CHANJO KWA MIFUGO,KANUNI/FORMULA NZURI ZA VYAKULA VYA MIFUGO TUNASIMAMIA MASHAMBA YA MIFUGO (FARM), TUNATOA MCHANGANUO WA FEDHA UNAOHUSIANA MIRADI YA UFUGAJI 0763222500

PATA MAARIFA FUGA TAJIRIKA

FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU.

FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU. Dume la Sungura linauwezo wa kutumika vizuri kwa kupandisha majike ya sungura baada ya miezi 8. Kabla ya kutimiza mwaka 1 Anaweza kupanda sungura  jike 1 kila baada ya siku 3 au 4. Na baada ya kufikia umri wa miezi 12 (mwaka1) na zaidi anauwezo wa kutumika kupandisha majike 4-6 ndani ya siku 7 (wiki1). Sungura madume waliozeeka wwnye umri kuanzia miaka 6 na zaidi hawatakiwi kutumika kwenye uzalishaji kwani ubora wa nguvu zao hupungua kufikia umri huo. Kitalaam unashauriwa kuhakikisha sungura wako wa mbegu anapata nyongeza ya chakula chenye virutubisho aina ya  protein, Vitamini na Madini  ili kuwafanya wawe na afya nzuri wakati wote. Pia unashauriwa kutowwka madume ya mbegu zaidi ya mmoja ndani chumba au banda moja kwa sababu madume wanatabia ya kupigana na kuumizana vibaya pindi wanapokaa pamoja. by Dr Riziki Ngogo FARMERS Platform 0763222500 0652515242 Follow zaidi http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http://www.facebook

JIWE LA MADINI/ MINERAL BLOCK

FARMERS PLATFORM PATA MAARIFA, FUGA, TIMIZA MALENGO Bonyeza hapa kutazama bidhaa Kwa nini Jiwe la Madini ni muhimu kwa Wanyama? Kwa kukosekana kwa chumvi chumvi na madini; hamu ya kula hupungua, ukuaji hupungua, uzalishaji wa maziwa na nyama hupungua, matatizo ya uzazi yanaweza kupatikana, mfumo wa kinga (mfumo wa ulinzi) hudhoofika na wanyama hushambuliwa na magonjwa. Kukosa madini haya kunaweza kupeleka tabia zifuatazo kwa wanyama; kula na kulamba vitu visivyo vya chakula (jiwe, udongo, mfupa, sachet, nguo, nk)  Wanyama hutumia  JIWE LA MADINI/ MINERAL BLOCK Mfululizo kwa ajili ya kufidia kiasi Cha madini kilichopungua mwilini. Kesi za kuhara zinazotokana na tabia hizi pia huzuiwa ikiwa mnyama atapata madini inavyopaswa. Kiasi cha Matumizi: matumizi ya kila siku kwa MINERAL BLOCK;  Ng'ombe kila siku 80 gr / siku,  Kondoo, mbuzi 5-15 gr / siku. Bonyeza hapa kutazama bidhaa Why Mineral Block in Animals? In the absence of salt and mineral matter; appetite decreases, growth slows, mi

MBOLEA/ FOLIAR FERTILIZERS

BONYEZA HAPA KUONA BIDHAA ZINGINE Kwanini mbolea ya Booster? Booster ni mbolea kamili ya mimea iliyo na virutubishi vyote muhimu kwa ukuaji wa mmea wenye afya na mavuno bora. Imetengenzwa  maalumu ili kuweza kufyonzwa haraka kupitia majani ya mmea. BONYEZA HAPA KUONA BIDHAA ZINGINE Why Booster Fertilizer? Booster is a complete foliar fertilizer containing all the major macro and microelements essential to healthy plant growth and optimum yields. Booster formulated for rapid absorption through the leaves. BONYEZA HAPA KUONA BIDHAA ZINGINE

ZUIA NG'OMBE KUNYONYA MAZIWA

Dairy Cow self suckling / Calf Suckling Milk Preventer (Antisuckling). ||●Easy to use no side effects ||●This tool is available in our store buy today KIFAA CHA KUZUIA NG'OMBE ANAEKAMULIWA KUJINYONYA MAZIWA AU NDAMA KUNYONYA MAZIWA. ||●Ni rahisi kutumia na hakina madhara yoyote. ||●Kinapatikana ndani ya Store zetu. By Dr NgogoR Vet FARMERS Platform 0763222500 #F #A #R #M #E #R #S Platform #farmersguidebook#FARMERS#Farmersplatform#FarmersConsultation#VeterinaryFreeConsultation#AnimalWelfare#AnimalCare#Mifugo#Ufugaji#KIENYEJI#MBWA#KUKU#CHANJO#MATITABU#LISHE#DAIRYFARMING

SABABU ZA KUKU KUNYONYOKA MANYOYA

_UFANISI WA KUKU_ Fahamu kuwa, kwa kawaida kuku hunyonyoka manyoya na kuota manyoya mapya  katika vipindi tofauti vya ukuaji wa kuku. *_Moulting_* Kunyonyoka manyoya na kubadilisha manyoya mapya hutokea kuku akiwa na umri wa kianzia wiki ya 4-5, wiki ya 8, Wiki ya 13, Wiki ya 20. Pia angalau mara moja kwa kila mwaka akifikia umri wa utagaji. Visababishi vingine vinavyochangia kunyonyoka manyoya na kuota manyoua mapya ni pamoja na _mabadiliko na upungufu wa chakula, mabadiliko ya kimsimu ya hali ya hewa, mabadiliko ya ghafla ya mwanga_ n.k Tambua kuwa kunyonyoka manyoya kunaweza kuathiri ufanisi wa kuku katika ukuaji/kuongezeka uzito na utagaji, hivyo unashauriwa kufanya yafuatayo, _1. Punguza stress kwa kuku._ _2. Tumia chakula bora chenye protein ya kutosha._ _3. Epuka mabadiliko ya ghafla kwenye mwanga, chakula n.k._ ●By Dr Riziki Ngogo      0763222500    #ReSta AgroVET    #FARMERS Platform    # INTERCHICK-  Chicken School of Excellence FARMERS PLATFORM PATA

Farmers Platform


Minyoo kwenye mbuzi (cyst from goat)

PLASTIC BAGS

PLASTIC BAGS
Mifuko ya plastiki ni hatari kwa mifugo yako. Huleta hasara na kushuka kwa uzalishaji wa kipato (Pile of bags more than 1Kg removed from one goat kama tunaweza kuona afya isiyoridhisha kwa huyu mbuzi

FRACTURE IN CATTLE

FRACTURE IN CATTLE
Management of fracture

UFUGAJI WA KUKU KWA TIJA

UFUGAJI WA KUKU KWA TIJA
KITABU CHA MWONGOZOUFUGAJI WA KUKU

UFUGAJI WA NGURUWE KWA TIJA

UFUGAJI WA NGURUWE KWA TIJA
KITABU CHA MWONGOZO BORA UFUGAJI WA NGURUWE, TENGENEZA FAIDA NDANI YA MUDA MFUPI

FUGA KWA TIJA

FUGA KWA TIJA
Fahamu kanuni za lishe bora kwa mifugo yako

MBINU ZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

MBINU ZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
MBINU ZA UFUGAJI

Mimea hii ni sumu kwa mifugo yetu husababisha vifo vya ghafla

Mastitis in goat