FAHAMU HATUA ZA UKUAJI WA MBWA NA HUDUMA MUHIMU HATUA KWA HATUA ✅ 1-4 Wiki *⃣Macho na masikio hufungua siku ya 10. *⃣Siku ya 15 mbwa anaweza kusimama. *⃣Siku ya 20 mbwa anaanza kujifunza kutembea. Watoto bado wanahitaji sana kuwa karibu na mama. *⃣Kwa Kawaida hata kama puppy mbwa mtoto ana afya. Chukua mtalamu wa mifugo siku ya 1 au 2 ili aangalie matatizo ya kuzaliwa. *⃣Mikia inaweza kukatwa katika umri huu. kucha zinaweza kukatwa pia *⃣Puppy mbwa mtoto anajifunza kuwa na uhusiano na mama na mahusiano ya karibu na wengine baadaye.
FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU. Dume la Sungura linauwezo wa kutumika vizuri kwa kupandisha majike ya sungura baada ya miezi 8. Kabla ya kutimiza mwaka 1 Anaweza kupanda sungura jike 1 kila baada ya siku 3 au 4. Na baada ya kufikia umri wa miezi 12 (mwaka1) na zaidi anauwezo wa kutumika kupandisha majike 4-6 ndani ya siku 7 (wiki1). Sungura madume waliozeeka wwnye umri kuanzia miaka 6 na zaidi hawatakiwi kutumika kwenye uzalishaji kwani ubora wa nguvu zao hupungua kufikia umri huo. Kitalaam unashauriwa kuhakikisha sungura wako wa mbegu anapata nyongeza ya chakula chenye virutubisho aina ya protein, Vitamini na Madini ili kuwafanya wawe na afya nzuri wakati wote. Pia unashauriwa kutowwka madume ya mbegu zaidi ya mmoja ndani chumba au banda moja kwa sababu madume wanatabia ya kupigana na kuumizana vibaya pindi wanapokaa pamoja. by Dr Riziki Ngogo FARMERS Platform 0763222500 0652515242 Follow zaidi http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http://www.facebook