UFUGAJI WA KUKU BORA WA MAYAI
SIKU YA 1 -5:
WAPE
GLUCOSE NA MCHANGANYIKO MMOJAWAPO KATI YA HII IFUATAYO:-
1. NEOXYVITAL AU OTC PLUS NA TYPHOPRIUM AU TRIMAZIN,
CHAKULA:
WEKA VIGOSTART AMBAYO INA RIDOCOX KWENYE CHAKULA, KILO MOJA KWA
MFUKO KUANZIA WIKI YA KWANZA HADI NNE ILI KUZUIA COCCIDIOSIS. BAADA YA KUACHA
KUACHA ENDELEA KUTUMIA RIDOCOX 200g/TANI
KWA KUZUIA COCCIDIOSIS HADI WANAPOANZA KUTAGA MAYAI.
SIKU YA 6:
VITAMINI(VITASTRESS.)
SIKU YA 7:
CHANJO YA NEWCASTE MASAA
MAWILI TU. WEKA MAJI YA VITAMINI (VITASTRESS) MARA BAADA YA KUTOA MAJI YA
CHANJO.
WIKI YA PILI:
CHANJO YA GUMBORO MASAA MAWILI TU. HALAFU ENDELEA NA MAJI YA VITAMIN
(VITASTRESS)
WIKI YA TATU:
DOXYCOL AU CTC 20% AU ANFLOX GOLD AU FLUBAN NA AMPROLIUM, VITALYTE AU VITASTRESS, MOLASSES KWA SIKU 5-7
WIKI YA NNE:
HAKIKISHA
KUKU WA NYAMA WANAKUWA KATIKA DOZI KUBWA YA VITAMINI (VITASTRESS)
WIKI YA TANO:
HAKIKISHA
KUKU WANAKUWA KATIKA DOZI NDOGO YA VITAMINI (VITASTRESS)
WIKI YA SITA:
WAPE KUKU MAJI YA VITAMINI ASUBUHI NA MATUPU JIONI.
WIKI YA NANE:
WAPE
KUKU WA MAYAI
- CHANJO YA NDUI
- DAWA YA MINYOO (PIPERAZINE AU LEVIWORM)
- VITAMINI (SUPERVIT LAYERS).
- WALISHE GROWERS MASH HADI MIEZI 3 ½. TUMIA LAYERS MASH WAKIFIKA MIEZI 4 KAMILI
- PIA HAKIKISHA WANAPATA CHAKULA CHENYE RIDOCOX HADI WANAPOANZA KUTAGA, PIA WAPE MAJANI.
WIKI YA 12:
- CHANJO YA NEWCASTLE (RUDIA KILA BAADA YA MIEZI 3). MASAA MAWILI KISHA WAPE MAJI YA VITAMINI
WIKI YA 16:
KATA MIDOMO KISHA WAPE NEOXYVITAL KWA SIKU 3-5. ANDAA VIOTA
KATA MIDOMO KISHA WAPE NEOXYVITAL KWA SIKU 3-5. ANDAA VIOTA
WIKI YA 48:
- WAPE VIRUTUBISHO VYENYE KUONGEZA WINGI WA MAYAI KAMA VILE G.L.P (KILO 1 KWA KILA KILO 50 ZA CHAKULA WIKI YA KWANZA NA ½ KILO KWA WIKI ZINAZOFUATA) NA VITAMINI.
WIKI YA 52:
- CHAGUA KUKU WASIO NA DALILI ZA KUTAGA KABISA, WENYE MAGONJWA SUGU NA WENYE TABIA ZISIZOFAA (VICES) WAUZE ILI KUPUNGUZA GHARAMA
WIKI YA 72:
- TUMIA V-RID KUSAFISHA MABANDA ILI KUUA VIJIDUDU. PIA WEKA MAJI YA DAWA HII KWENYE KISAFISHA MIGUU (FOOTBATH) ILI KUHAKIKISHA UDHIBITI WA VIJIDUDU (BIOSECURITY) NA KWAMBA VIFARANGA WANAOWEKWA HAWAATHIRIWI NA VIJIDUDU HIVYO
WIKI YA 96:
ONDOA
KUKU WOTE WALIOZEEKA☎📞Riziki Ngogo(Vet Dr)
AfyaMIFUGO Tz
0763222500/0652515242
afyamifugo.blogspot.com
afyamifugo@gmail.com
Maoni
Chapisha Maoni