*UFUGAJI WA NYUKI KWENYE MIZINGA*
🐝🐝🐝🐝🐝🐝🐝
Nyuki ni chanzo cha uzalishaji wa asali
🐝Ufugaji nyuki (au *apiculture*, jina limetokana na neno la Kilatini apis= nyuki)
🐝Apiculture ni ufugaji wa nyuki wa asali unaohusisha utengenezaji wa mizinga ya nyuki, mara nyingi ikiwa ni pamoja na kuwazalisha nyuki kwa makundi toafauti tofauti.
🐝 Mfugaji wa nyuki (au apiarist) hufuga nyuki ili kukusanya asali na bidhaa nyingine zitikanazo na ufugaji wa nyuki.
🐝Eneo ambapo nyuki wanahifadhiwa au kufugwa huitwa "apiary"
🐝Asali hutumika kama chakula pia inajulikana kuwa na thamani ya dawa. Inajulikana kuwa muhimu sana katika matibabu ya matatizo mbalimbali ya wanadamu kuhusiana na mmeng'enyo wa chakula yaani digestion, ugonjwa wa kuhara kutapika, magonjwa ya tumbo na ugonjwa wa ini.
🐝 Utafiti wa kisasa unaonyesha kwamba asali:
🐝Inazuia ukuaji wa bakteria ya mdomo Inatengeneza layer mdomoni na kwenye koo na hupunguza vidonda kooni. Pia asali hutumiwa katika matibabu ya vidonda vya tumbo au peptic. Asali Inafaa katika matibabu ya majeraha na maambukizi mbalimbali kwa sababu ya uwezo wake wa kuwa antimicrobial (antibacterial, antiviral and antifungal).
🐝Pia Asali inatumika kama antioxidant. Hii ina maana kwamba inaruhusu damu kuenea vizuri na kutoa oksijeni zaidi kwenye maeneo ya mwili kama vile ubongo.
🐝Inaweza pia kutumika nje ya mwili kwenye ngozi ili kukuza uponyaji inapotumika kwenye majeraha, hata majeraha ya baada ya operation ndogo.
Inatumika pia mahali penye majeraha ya moto.
🐝Asali Ina aina ya sukari na madini na imeonyeshwa kuwa na kiwango kidogo cha kalori na inafaa kama sweetener kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari, watu walio na ugonjwa wa moyo au wale ambao ni overweight.
🐝Ufugaji wa nyuki pia husaidia katika matumizi mengine ya kilimo kama Uchavushaji wa maua ya mimea, kwani pollens huhamishwa kutoka maua ya sehemu moja hadi nyingine na nyuki wakati wanapokusanya nectari.
UFUGAJI WA NYUKI HUSAIDIA KUTUNZA MAZINGIRA TUFUGE NYUKI WA ASALI KWA WINGI.
BILA NYUKI HATUPATI CHAKULA CHA KUTOSHA YAANI HATUTAPATA ASALI PIA BILA NYUKI HATUTAPATA MAZAO YA KUTOSHA KUTOKANA NA KUPUNGUA KWA UCHAVUSHAJI WA MIMEA.
*Jiunge nasi.....*
*Itaendelea*
Dr Riziki Ngogo (Vet)
*AfyaMIFUGO Tz*
afyamifugo.blogspot.com
0763222500 whatsap
0652515242
afyamifugo@gmail.com
Veterinary services and animal care: facebook
afya_mifugo_tz : instagram
Asantee Kaka nimejifunza mengi
JibuFutaTunashukura kwa comment yako ndugu karibu sana
JibuFutaTunashukura kwa comment yako ndugu karibu sana
JibuFuta