*FAHAMU UMUHIMU WA DCP KWA MIFUGO.* DCP=Dicalcium Phosphate ✅*DCP ni nini ?* DCP ni mchanganyiko wa madini ya Calcium na Phosphorus. DCP husaidia wanyama wenye upungufu au maradhi yatokanayo na ukosefu wa madini haya ya Calcium na Phosphorus ✅FAIDA KWA KUKU: Huzuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini, huimarisha maganda ya mayai, Pia husaidia utagaji wa mayai ✅FAIDA KWA WANYAMA WENGINE: Huzuia ng’ombe kuanguka, viungo dhaifu na huimarisha mifupa na kupunguza matatizo ya mifupa. 📞Dr Riziki Ngogo(DVM) ☎*AfyaMIFUGO Tz* 0763222500 afyamifugo@gmail.com afyamifugo.blogspot.com
FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU. Dume la Sungura linauwezo wa kutumika vizuri kwa kupandisha majike ya sungura baada ya miezi 8. Kabla ya kutimiza mwaka 1 Anaweza kupanda sungura jike 1 kila baada ya siku 3 au 4. Na baada ya kufikia umri wa miezi 12 (mwaka1) na zaidi anauwezo wa kutumika kupandisha majike 4-6 ndani ya siku 7 (wiki1). Sungura madume waliozeeka wwnye umri kuanzia miaka 6 na zaidi hawatakiwi kutumika kwenye uzalishaji kwani ubora wa nguvu zao hupungua kufikia umri huo. Kitalaam unashauriwa kuhakikisha sungura wako wa mbegu anapata nyongeza ya chakula chenye virutubisho aina ya protein, Vitamini na Madini ili kuwafanya wawe na afya nzuri wakati wote. Pia unashauriwa kutowwka madume ya mbegu zaidi ya mmoja ndani chumba au banda moja kwa sababu madume wanatabia ya kupigana na kuumizana vibaya pindi wanapokaa pamoja. by Dr Riziki Ngogo FARMERS Platform 0763222500 0652515242 Follow zaidi http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http://www.facebook