Sungura Aina ya CHINCHILLA ni Aina ya sungura wapole na watulivu wenye sifa zifuatazo. ■Wanafugika vizuri ■Wapole na wavumilivu ■Wanauwezo wa kuzaa watoto 6-9 ■Wana rangi ya kijivu iliyokolea ■Wanakua haraka ■Wanauwezo mkubwa wa kulea watoto ■Wanaweza kutumika kwa nyama, manyoya, Mkojo wao na kinyesi chao na kama pambo nyumbani. Wanaweza kuishi kwa miaka 5-8 ■Wastani wa uzito wao wakiwa wakubwa kilo 4- 5.5Kg. Jifunze zaidi kila siku kupitia kurasa zetu http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http://www.facebook.com/farmersplatform/ http://www.instagram.com/farmers_platform/ KARIBU UJIPATIE SUNGURA BORA NA HUDUMA BORA ZA KITAALAM. Dr NgogoR 0763222500 Farmers Platform PATA MAARIFA FUGA TAJIRIKA ~SHARE NA WAFUGAJI WENZAKO~
FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU. Dume la Sungura linauwezo wa kutumika vizuri kwa kupandisha majike ya sungura baada ya miezi 8. Kabla ya kutimiza mwaka 1 Anaweza kupanda sungura jike 1 kila baada ya siku 3 au 4. Na baada ya kufikia umri wa miezi 12 (mwaka1) na zaidi anauwezo wa kutumika kupandisha majike 4-6 ndani ya siku 7 (wiki1). Sungura madume waliozeeka wwnye umri kuanzia miaka 6 na zaidi hawatakiwi kutumika kwenye uzalishaji kwani ubora wa nguvu zao hupungua kufikia umri huo. Kitalaam unashauriwa kuhakikisha sungura wako wa mbegu anapata nyongeza ya chakula chenye virutubisho aina ya protein, Vitamini na Madini ili kuwafanya wawe na afya nzuri wakati wote. Pia unashauriwa kutowwka madume ya mbegu zaidi ya mmoja ndani chumba au banda moja kwa sababu madume wanatabia ya kupigana na kuumizana vibaya pindi wanapokaa pamoja. by Dr Riziki Ngogo FARMERS Platform 0763222500 0652515242 Follow zaidi http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http://www.facebook