*KWA WAFUGAJI SOMA HII, PATA MAARIFA KUHUSU VITU VINAVYOWEZA KUKUONGEZEA FAIDA KWENYE KAZI YA UFUGAJI .* *(AI) UHAMILISHAJI/ Artificial Insemination* inajulikana kwa wafugaji wengi kama AI, ni moja ya mbinu za kuzaliana ambazo zimechangia katika maendeleo ya sekta mifugo hasa katuka sekta ya maziwa katika nchi zilizofanikiwa kwenye ufygaji wenye tija na faida kubwa. Mbinu ya AI huanza na kuchagua ng'ombe wenye afya nzuri, ambao hawana ugonjwa wala kilema cha aina yoyote na wenye uwezo wa kuzalisha mazoa yake kwa kiasi kikubwa cha ubora wa juu. Wafugaji/ Wakulima wanashauriwa kutumia mbegu zilizothibitika kutoka kwa mifugo wazazi walio thibitika ambao wanapatikana kutoka vituo vya AI na watoa huduma waliosajiliwa. ✅ *Faida za Uhamilishaji/AI* 1.Kuzuia magonjwa yanayoweza kuenezwa kutoka kwa dume. 2.Kiasi cha mbegu nyingi kinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu na kwa gharama ndogo ili kuwezesha upimaji mkubwa na uteuzi wa ng'ombe bora. 3.Inaimarisha na kuboresha maen...
_UFANISI WA KUKU_ Fahamu kuwa, kwa kawaida kuku hunyonyoka manyoya na kuota manyoya mapya katika vipindi tofauti vya ukuaji wa kuku. *_Moulting_* Kunyonyoka manyoya na kubadilisha manyoya mapya hutokea kuku akiwa na umri wa kianzia wiki ya 4-5, wiki ya 8, Wiki ya 13, Wiki ya 20. Pia angalau mara moja kwa kila mwaka akifikia umri wa utagaji. Visababishi vingine vinavyochangia kunyonyoka manyoya na kuota manyoua mapya ni pamoja na _mabadiliko na upungufu wa chakula, mabadiliko ya kimsimu ya hali ya hewa, mabadiliko ya ghafla ya mwanga_ n.k Tambua kuwa kunyonyoka manyoya kunaweza kuathiri ufanisi wa kuku katika ukuaji/kuongezeka uzito na utagaji, hivyo unashauriwa kufanya yafuatayo, _1. Punguza stress kwa kuku._ _2. Tumia chakula bora chenye protein ya kutosha._ _3. Epuka mabadiliko ya ghafla kwenye mwanga, chakula n.k._ ●By Dr Riziki Ngogo 0763222500 #ReSta AgroVET #FARMERS Platform # INTERCHICK- ...