Trichinella spiralis. MINYOO HATARI KWA BINADAMU, HATARI KWA WANYAMA Trichinella spiralis ni minyoo aina ya nematode inayopatikana kwenye panya, nguruwe, fisi na wanadamu, na inasababisha ugonjwa wa trichinosis. Wakati mwingine huitwa "minyoo ya nguruwe" kwa sababu mara nyingi hupatikana kwenye nyama ya nguruwe, na binadamu anaweza kuipata minyoo hio kwa kula nyama ya nguruwe mwenye minyoo ambaye haijaivishwa vizuri. USHAURI. Mfugaji wa nguruwe hakikisha unafuga nguruwe kwa kufuata taratibu za afya ya mifugo wape dawa ya minyoo nguruwe wako kwa wakati. Muuzaji wa nyama ya nguruwe hakikisha unauza nyama iliyopimwa na wataalamu wa afya ya mifigo (Meat Inspectors) Pia Wanunuzi wa nguruwe hakikisha unanunua nguruwe mwenye afya nzuri aliyefanyiwa uchunguzi na Daktari wa mifugo ili kuweza kupata nguruwe wa nyama asiyekuwa na minyoo. Wataalamu wa mofugo hakikisha nyama ya nguruwe inayouzwa katika eneo lako imepimwa na mkaguzi wa nyama. Linda Afya ya Mifugo Linda A...
_UFANISI WA KUKU_ Fahamu kuwa, kwa kawaida kuku hunyonyoka manyoya na kuota manyoya mapya katika vipindi tofauti vya ukuaji wa kuku. *_Moulting_* Kunyonyoka manyoya na kubadilisha manyoya mapya hutokea kuku akiwa na umri wa kianzia wiki ya 4-5, wiki ya 8, Wiki ya 13, Wiki ya 20. Pia angalau mara moja kwa kila mwaka akifikia umri wa utagaji. Visababishi vingine vinavyochangia kunyonyoka manyoya na kuota manyoua mapya ni pamoja na _mabadiliko na upungufu wa chakula, mabadiliko ya kimsimu ya hali ya hewa, mabadiliko ya ghafla ya mwanga_ n.k Tambua kuwa kunyonyoka manyoya kunaweza kuathiri ufanisi wa kuku katika ukuaji/kuongezeka uzito na utagaji, hivyo unashauriwa kufanya yafuatayo, _1. Punguza stress kwa kuku._ _2. Tumia chakula bora chenye protein ya kutosha._ _3. Epuka mabadiliko ya ghafla kwenye mwanga, chakula n.k._ ●By Dr Riziki Ngogo 0763222500 #ReSta AgroVET #FARMERS Platform # INTERCHICK- ...