_UFANISI WA KUKU_ Fahamu kuwa, kwa kawaida kuku hunyonyoka manyoya na kuota manyoya mapya katika vipindi tofauti vya ukuaji wa kuku. *_Moulting_* Kunyonyoka manyoya na kubadilisha manyoya mapya hutokea kuku akiwa na umri wa kianzia wiki ya 4-5, wiki ya 8, Wiki ya 13, Wiki ya 20. Pia angalau mara moja kwa kila mwaka akifikia umri wa utagaji. Visababishi vingine vinavyochangia kunyonyoka manyoya na kuota manyoua mapya ni pamoja na _mabadiliko na upungufu wa chakula, mabadiliko ya kimsimu ya hali ya hewa, mabadiliko ya ghafla ya mwanga_ n.k Tambua kuwa kunyonyoka manyoya kunaweza kuathiri ufanisi wa kuku katika ukuaji/kuongezeka uzito na utagaji, hivyo unashauriwa kufanya yafuatayo, _1. Punguza stress kwa kuku._ _2. Tumia chakula bora chenye protein ya kutosha._ _3. Epuka mabadiliko ya ghafla kwenye mwanga, chakula n.k._ ●By Dr Riziki Ngogo 0763222500 #ReSta AgroVET #FARMERS Platform # INTERCHICK- Chicken School of Excellence FARMERS PLATFORM PATA
FAHAMU KUHUSU DUME LA SUNGURA LA MBEGU. Dume la Sungura linauwezo wa kutumika vizuri kwa kupandisha majike ya sungura baada ya miezi 8. Kabla ya kutimiza mwaka 1 Anaweza kupanda sungura jike 1 kila baada ya siku 3 au 4. Na baada ya kufikia umri wa miezi 12 (mwaka1) na zaidi anauwezo wa kutumika kupandisha majike 4-6 ndani ya siku 7 (wiki1). Sungura madume waliozeeka wwnye umri kuanzia miaka 6 na zaidi hawatakiwi kutumika kwenye uzalishaji kwani ubora wa nguvu zao hupungua kufikia umri huo. Kitalaam unashauriwa kuhakikisha sungura wako wa mbegu anapata nyongeza ya chakula chenye virutubisho aina ya protein, Vitamini na Madini ili kuwafanya wawe na afya nzuri wakati wote. Pia unashauriwa kutowwka madume ya mbegu zaidi ya mmoja ndani chumba au banda moja kwa sababu madume wanatabia ya kupigana na kuumizana vibaya pindi wanapokaa pamoja. by Dr Riziki Ngogo FARMERS Platform 0763222500 0652515242 Follow zaidi http://www.afyamifugo.blogspot.com/ http://www.facebook